MWANZO MPYA WA YANGA SC

YANGA SC BINGWA NGAO YA JAMII

YANGA wameanza 2024/25 kwa kutwaa taji la Ngao ya Jamii baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Mkapa Agosti 11 2024 ikiwa ni balaa lao kwenye kutwaa mataji yanayokuwa mbele yao.

Katika fainali ambayo ilianza kwa kasi kubwa ni mabao matano yamefungwa kwenye fainali huku kila bao likitoka kwa mfungaji mmojammoja kwenye fainali yakibabe.

Feisal Salum alianza kufunga bao dakika ya 13 kwa Azam FC lilikuwa ni bao pekee kwa Azam FC mpaka mwisho wa mchezo huku Prince Dube akiweka usawa dakika ya 18, Boka dakika ya 27, Aziz Ki dakika ya 30 na msumari wa mwisho ni mali ya Mzize Clement dakika ya 90.

Dube amesema ni furaha kubwa kutwaa taji la Ngao ya Jamii kwa kuwa walishirikiana kufanya kazi kubwa uwanjani na mwisho wakatwaa taji hilo.

“Furaha kubwa kufunga na ilikuwa kazi nzuri kutoka kwa Mudathir Yahya ambaye tulikuwa tunafanya naye kazi ndani ya Azam FC hivyo ni mwendelezo wa kile ambacho tulikuwa tunakifanya na ninapenda kuona inakuwa hivi.”

0/Post a Comment/Comments